1 Kor 12:7 “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.”
MUHTASARI. Roho Mtakatifu
anadhihirisha kupitia karama mbali mbali za rohoni walizokirimiwa waumini
(1 Kor 12:7). Udhuhirisho huo wa Roho umekusudiwa kulijenga na kulisafisha
kanisa (1 Kor 12:7 tazama 14:26, maelezo). Karama hizi za Rohoni sio sawa na karama
za huduma zilizooneshwa katika Rum 12:6-8 na Efe 4:11, ambapo mwumini anapokea
nguvu na uwezo wa kudumu katika kanisa. Orodha ilioko katika 1 Kor 12:8-10
haina mana kuwa inataja mambo yote , na kuwa karama zinaweza kutenda kazi
katika michanganyiko ya namna mbali mbali.
1.
Udhihirisho wa utendaji wa Roho
hufanyika kulingana na mapenzi ya Roho mwenyewe (1Kor 12:11) pale inapohitajika
na kulingana na shauku ya mwamini.(12:31,14:1)
2.
Baadhi ya karama zinaweza
kudhihirishwa kwa kupitia mtu fulani mara kwa mara na inawezakana mwumini
kutumiwa kwa karama zaidi ya mojaili kuhudumu kulingana na mahitaji yaliyopo.
Muumini anatakiwa kutamani “karama mbali mbali” na si moja tu (1 kor
12:31;14:1)
3.
Si kulingana na Maandiko na wala si
hekima kuchukulia kwamba kwa sababu mtu anatumiwa katika karama inayoonekana
sana,kuwa mtu huyu ni wa kiroho zaidi ya yule anayetumiwa katika karama
zisizoonekana sana .
4.
Udhihirisho wa Roho Mtakatifu kwa
nia ya karama unaweza kughushiwa na Shetani au watendajibandia wanaojifanya
kuwa watumishi wa Kristo (Mt 7:21-23,24:11,24. 2 Kor11:13-15; 2 Thes 2:8-10).
Mwamini hapasi kuamini kila udhihirisho wa Roho, lakini anashauriwa
“zijaribuni hizi roho, kwamba zimetokana na Mungu, kwa sababu manabii wa
uongo wengi wametokea duniani” (1 Yoh 4:1;1Thes 5:20-21; tazama makala juu ya
KUPIMA UBATIZO WA KWELI KATIKA ROHO MTAKATIFU, uk. 1758.
KARAMA
MOJA MOJA. Katika 1Kor 12:8-10, Paulo anadhihirisha karama mbali
mbali ambazo Roho Mtakatifu hukirimia waumini. Ijapokuwa haelezei hapa jinsi
zilivyo, tunaweza kukusanya maelezo ya hapa na pale kutoka aya zingine kujua
zitakuaje.
1.
Neno la Hekima.
Hili ni matamashi ya hekima
yanyosemwa kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu.Huleta ufunuo wa Neno la
Mungu au hekima ya Roho Mtakatifu kwa tukio maalum au tatizo (Mdo 6:10;
15:13-22). Hata hivyo, si sawa na kuwa na hekima ya Mungu kwa ajili ya
maisha ya kila siku. Neno la hekima linakuja kwa kulisoma Neno la
Mungu kwa bidii na kutafakari njia za Mungu na Neno lake, na kwa
kuomba (Yos 1:5-6).
2.
Neno la
Maarifa. Hili ni matamshiyaliyovuviwa na
Roho Mtakatifu yanayoleta ufunuo wa ufahamu kuhusu watu, mazingira, au kweli ya
Biblia. Mara nyingi limekuwa na uhusiano wakaribu na unabii (mdo
5:1-10;10:47-48;15:7-11;1Kor 14:24-25)
3.
Imani. Hii sio imani inayookoa, lakini imani mahsusi inayatoka kwa
Mungu na kuletwa na Roho Mtakatifu inayomwezesha Mkristo kumwamini Mungu
matendo yasiyo ya kawaida ya miujiza . ni imani inayohamisha milima (1 Kor
13:2) na mara nyingi inaonekana ikitenda kazi pamoja na karama zingine kama
vile uponyaji na matendo ya miujiza (taz. Mt 17:20, maelezo juu ya imani ya
kweli;Mk 11:22-24;Lk 17:6)
4.
Karama za
Uponyaji. Karama hizi zinatolewa kwa
kanisa ili kuweza kurejesha afya katika mwili kwa njia ya muujiza (Mt
4:23-25;10:1;Mdo 3:6-8;4:30).Ule wingi “karama “ unaashiria uponyaji wa
magonjwa mbali mbali na kuonyesha kuwa kila tendo la uponyaji ni karama
maalum kutoka kwa Mungu . Ijapokuwa karama ya uponyaji haitolewi kwa kila mmoja
katika kanisa kwa njia maalum (ling 1Kor 12:11,30),waumini wote
wanaweza kuombea wagonjwa. Mahali palipo na imani wagonjwa
watapona (taz. Makala juu ya UPONYAJI WA KIMUNGU,UK.1502).Uponyaji
unaweza kuja kama matokeo ya kutii maelekezo ya Yos 5:14-16(taz.Yos 5:14-16
maelezo).
5.
Matendo ya
Miujiza. Haya ni matendoyanayotoletwa na
nguvu za Mungu mwenyewe yanayobadilisha mwenendo wa kawaida wa mambo ya asili.
Ni pamoja na matendo ya nguvu za Mungu ambapo ufalme wa Mungu unadhihirishwa
dhidi ya Shetani na pepo wabaya (taz. Yn 6:2, maelezo;taz. Makala juu ya UFALME
WA MUNGU, uk.1510).
6.
Unabii. Inatupasa kutofautisha kati ya unabii kama udhihirisho wa
muda tu wa Roho.(1 Kor 12:10) na unabii kama karama na huduma ya
kanisa(Efe 4:11).kama karama ya huduma, karama ya unabii inakirimiwa kwa baadhi
ya waamini tu, ambao hawana budi kufanya kazi kama manabii ndani ya Kanisa
(taz. Makala juu ya KARAMA ZA HUDUMA ZA KANISA,uk.1928) kama udhihirisho wa
kiroho, unabii ni karama inayoweza kupatikana kwa kila Mkristo aliyejazwa Roho
Mtakatifu (Mdo 2:17-18)
Kuhusu
utabiri au unabii kama udhihirishowa kiroho:(a )unabii ni karama maalumu
inayomwezesha kuleta neno la ufunuo moja kwa moja toka kwa Mungu kwa msukumo wa
Roho Mtakatifu (1 Kor 14:24-25;29-31). Unabii hapa sio kuleta ujumbe au
mahubiri yanyotayarishwa awali. (b) Katika Aj na Aj, unabii kimsingi si
kutabiri mambo yajayo baadaye, lakini kuyatangaza mapenzi ya Mungu na kuwaonya
na kuwatia moyo watu wa Mungu kuifuata haki, uaminifu na uvumilivu (14:3;taz.
Makala juu ya NABII KATIKA AGANO LA KALE,uk.1054). (c)Ujumbe huu unawezakuweka
wazi hali ya moyo wa mtu (14:25) au kuleta hali ya kuimarisha ,kutia
moyo,kufariji,kuonya na hukumu(14:3’25-26’31).(d) kanisa halipaswi kupokea
ujumbe wa unabii kuwa usio na mapungufu yoyote, kwqa sababu manabii wengi wa
uongo wataingia katika kanisa(1Yoh4:1). Hivyo, unabii wote hauna budi
kujaribiwa ili kuthibitisha uhalisi wake wa ukweli ( 1 kor 14:29,32;1 The
5:20-21)kwa kujiuliza kama unabii unalingana na Neno la Mungu (1 Yoh 4:1),
iwapo unasisitiza maisha ya kumcha Mungu (1 Tim 6:3), na iwapo umesemwa na mtu
anayeisha ya uaminifu katika Bwana Kristo (1 Kor 12:3). (e)unabii
unatenda kazi katika mapenzi ya Mungu na si ,mapenzi ya wanadamu. Aj halioneshi
kama lilijihusisha kwa bidii kutafuta ufunuo au uongozi kwa wale wanaodai kuwa
manabii. Unabii ulitolewa kwa kanisa pale tu,Mungu alikua chanzo cha ujumbe huo
(1Kor 12:11;2 Pet1:21).
7.
Kupambanua
Roho. Karama hii ni uwezo maalum
uliotolewa na Roho ili kwa uhakika kuweza kutambua na kupima unabii na
kupambanua iwapo unabii huo umetoka kwa Roho Mtakatifu au sivyo (taz.1
Kor 14:29, maelezo;1 Yoh 4:1).Wakati mwisho unakaribia watakapojitokeza walimu
wa uongo wengi (taz.Mt 24:5, maelezo) na upotoshaji wa Ukristo unaofuata Biblia
utongezeka sana (taz.1 Tim 4:1,maelezo), karama hii itakuwa ya muhimu sana kwa
Kanisa.
8.
Kunena kwa
Lugha. Kwa habari ya “lugha” (Gk
glossa,linalomaanishalugha)kama udhihirisho wa Roho,mambo yafuatayohayana budi
kuzingatiwa:
a.
Kunena kwa lugha kunaweza kuwa
katika lugha kunaweza kuwa katika lugha zinazozungumzwa sasa (Mdo 2:4-6)
au lugha isiyojulikana duniani, k.m lugha…za malaika” (1 Kor 13:1; taz.sura ya
14, maelezo;taz.makala juu ya KUONEKANA KWA LUGHA,uk.1734).Usemi wa jinsi hii
hautokani na kujifunza na mara nyingi haueleweki kwake anenaye (14:14) na
kwa wale wanaosikia (14:16).
b.
Kunena kwa lugha hujumuisha
roho ya binadamu na Roho wa Mungu kuingiliana ili mwumini aweze kuwasiliana na
Mungu moja kwa moja (yaani, katika maombi,kusifu, Baraka au shukrani),
kuonyesha au kutamka katika ya ngazi ya roho ya mtu badala ya akili ,(1Kor
14:2,14) na kujiombea mwenyewe au kuwaombea wengine kwa msukumo wa moja kwa
moja wa roho Mtakatifu mbali ya shughuli zinazoendelea katika akili(ling.1Kor
14:2 ,15,28;Yuda 1:20)
c.
Kunena kwa lugha katika kusanyiko ni
lazima kuambatane na tafsiri iliyotolewa na Roho mwenyewe, ambayo inaleta
yanayozungumzwa na maana ya matamshi yenyewe kwa jamii ya waaumini .(
1Kor 14:3,27-28). Ujumbe wake unaweza kuwa wa ufunuo,ufahamu, unabii au
mafundisho kwa ajili ya kusanyiko(ling.1Kor 14:6)
d.
Kunena kwa lugha katika kusanyiko
lazima kufanyike kwa utaratibu. Anayenena hatakiwi “kutekwa na hisia” au “
kushindwa kujidhibiti”(1Kor 14:27-28;taz. Makala juu ya KUNENA KWA LUGHA,uk
1734).
9.
Tafsiri ya
lugha. Huu ni uwezo unaotolewana Roho
mwenyewe wa kuelewa na kueleza maana ya maneno yayonenwa katika lugha .
Pale yanapofasiriwa kwa ajili ya kusanyiko, lugha hufanya kazi ya kutoa
mwongozo wa kuabudu na kuomba au kama unabii. Jumuiya ya waumini ndipo
inaponewa kushiriki katika ufunuo huu uliovuviwa na Roho Mtakatifu. Lugha
zilizofasiriwa zinaweza kuwa njia ya kujenga wakati kusanyiko zima linapopokea
usemi huo (ling.14:6,13)Karama anaweza kupewa Yule anenaye kwa lugha au mtu
mwingine. Wale wanenao kwa lugha inawapa pia kuomba karama ya utafsiri (1
Kor 14;:13)
KWA MAFUNDISHO MENGINE MAZURI ZAIDI HAKIKISHA UNATEMBELEA MTANDAO HUU
WA HEMA LA UFUNUO KILA SIKU KUJIFUNZA.







0 comments:
Post a Comment